Our Terms of Use and Privacy Policy have changed. We think you'll like them better this way.

DENZEL HOSTS RADIO VETERAN LEONARD MBOTELA "JE, HUU NI UNGWANA...???"

  • Broadcast in Social Networking
Denzel Musumba

Denzel Musumba

×  

Follow This Show

If you liked this show, you should follow Denzel Musumba.
h:106267
s:1066697
archived
Je,huu ni ungwana...??? Leonard "Mambo“ Mbotela ni mtangazaji mashuhuri wa redio nchini Kenya. Amejulikana kote nchini kutokana na huduma yake ya zaidi ya miaka 40 tangu 1964. Alikuwa mtangazaji wa habari na michezo hasa soka. Tangu 1966 amekuwa hewani na programu yake "Je, hii ni ungwana?". Leonard Mbotela alizaliwa huko Freretown, Mombasa katika familia ya kianglikana ya watoto nane. Babake James Mbotela alikuwa kati ya walimu wa kwanza Waafrika katika Kenya, mamake Ida alifanya kazi ya ustawi wa jamii. Leonard alisoma shule ya msingi ya Freretown kati ya 1948 na 1953 halafu Buxton shule ya kati Mombasa 1954 hadi 1958 akaendelea shule ya sekondari ya Kitui High School 1959 hadi 1963. Alipata nafasi ya kuingia katika ukurufunzi wa Sauti ya Kenya akishirikiana na Simon Ndesanjo katika programu ‘Hodi hodi mitaani’. 1964 aliajiriwa kama mtangazaji wa huduma ya Kiswahili. Mbotela alianzisha programu yake ya ‘Salamu za vijana’ pia akasoma taarifa za habari za huduma ya Kiswahili. Mwaka 1966 alianzisha ‘Je, huu ni ungwana?’ ambayo ni programu ya pekee inayoendelea hadi leo (2006). Alijulikana zaidi nchini kama mtangazaji wa soka kuanzia mwaka 1967. Kati ya programu zake zilizopendwa ni Uhalifu Haulipi, Ongea Lugha Sanifu and Waliosifika. Wakati wa uasi wa 1982 (jaribio la kijeshi la kupindua serikali ya rais Moi) Mbotela alilazimishwa kusoma habari za waasi kwa sababu sauti yake ilijulikana kote nchini. Katika maisha yake ya kazi alikuwa pia mhusika wa huduma ya "Presidential Press Service" chini ya Rais Moi kwa miaka saba. Alirudi KBC akastaafu mwaka 1997 akiwa na cheo cha mwangalizi mkuu wa programu za redio. Hata baada ya kustaafu ameendelea kusikika redioni akisoma habari na programu yake "Je hii ni ungwana?". Mbotela amemwoa Alice Mwikali mwaka 1970 akazaa naye watoto 3 : Ida, Jimmy na George.

Comments