Our Terms of Use and Privacy Policy have changed. We think you'll like them better this way.

MICHANGO ZA SHEREHE MBALI MBALI

  • Broadcast in Social Networking
Denzel Musumba

Denzel Musumba

×  

Follow This Show

If you liked this show, you should follow Denzel Musumba.
h:106267
s:1388585
archived
Dr. Olomi, Wazo lako ni la msingi sana, jamii ya kitanzania tunatakiwa tuanze kuangalia mambo kwa kutokea angle nyingine zaidi ya ile tuliyozoea. Yapo mabadiliko mengi yanayotokea na sisi yanatukumba lakini vile vile na sisi tubadilike ili tulete mabadiliko mengi zaidi kuboresha maisha na nchi yetu. Kubadili katiba ni namba moja, tume ya uchaguzi mbili, .... tatu, .... nne lakini na hili sijuhi ni la ngapi lakini ni muhimu kama mengine tunayoyatajaja. Nimekuwa nafuatilia jinsi desturi ya kuchangia na kufanya sherehe kubwa inavyozidi kushika kasi, ikipelekea ule wigo wa kuomba michango kupanuka kiasi kwamba sasa hata mtu ambaye jina lako halijui vizuri anaweza kukuomba mchango. Aidha michango na sherehe hizi zimekuwa mzigo mkubwa sana kwa baadhi ya watu, ikiwa ni pamoja na wale wenye kipato kidogo wanaochangiwa na kulazimika kulipa michango hiyo kwa miaka mingi. Je, wajua kuwa kuna familia ambazo zimefikia kulazimisha ndugu wauze mashamba au mifugo mtaji ili kupata fedha za kuchangia sherehe?. Je, wajua kuwa kuna watu ambao zaidi ya nusu ya kipato chao wanatumia kuchangia sherehe na huku wakishindwa kulipia huduma muhimu kama shule, matibabu, lishe, nk. Na kuwa wakati mwingine wewe au mimi (au wengine kama mimi na wewe) ndio wenyeviti na makatibu wa sherehe hiyo?. Na ni sisi tunaoona fahari ya kutumia milioni 30 au zaidi kwenye sherehe usiku mmoja? Kuna kijana mmoja jamaa yetu juzi juzi alipata shule Australia akawa anatafuta mchango wa dola 5,000 aende. Alipata 2,000 na amwekwama kwenda. Mwaka kesho akisema anaoa tutamchangia milioni 15-20!!!. Hii si hadithi, ni ukweli, na ni kielelezo cha ulimbukeni tuliofikia. Siku za karibuni nimetambua kuwa kuna kundi kubwa tu linasikitishwa na huu mwenendo, na hata kutambua kuwa tunaweza kuwa tunaandikiwa dhambi kubwa (na hukumu yatusubiri) kwa jinsi wengi wetu tunashindwa kusaidia mambo ya msingi lakini tunakuwa wepesi kutoa kwenye sherehe.

Facebook comments

Available when logged-in to Facebook and if Targeting Cookies are enabled