• 01:30

  MIAKA OURETTO EN FRANCE

  in News

  UNE EMISSION DE: AZO K.

 • 01:55

  MIAKA OURETTO SUR LE PLATEAU DE PAROLES ET VERITES

  in News

  UNE EMISSION PRESENTEE PAR JEANNETTE DICK  

 • 01:59

  PAROLES ET VERITES avec JEANNETTE DICK

  in News

  Emission animee et presentee par: JEANNETTE DICK "REACTIONS AUX DECLARATIONS DE MR FRANCOIS GUINA Conseiller Special de Mr MIAKA O.

 • 04:00

  MICHANGO ZA SHEREHE MBALI MBALI

  in Social Networking

  Dr. Olomi,

  Wazo lako ni la msingi sana, jamii ya kitanzania tunatakiwa tuanze kuangalia
  mambo kwa kutokea angle nyingine zaidi ya ile tuliyozoea.

  Yapo mabadiliko mengi yanayotokea na sisi yanatukumba lakini vile vile na sisi
  tubadilike ili tulete mabadiliko mengi zaidi kuboresha maisha na nchi yetu.

  Kubadili katiba ni namba moja, tume ya uchaguzi mbili, .... tatu, .... nne
  lakini na hili sijuhi ni la ngapi lakini ni muhimu kama mengine tunayoyatajaja.
  Nimekuwa nafuatilia jinsi desturi ya kuchangia na kufanya sherehe kubwa
  inavyozidi kushika kasi, ikipelekea ule wigo wa kuomba michango kupanuka
  kiasi kwamba sasa hata mtu ambaye jina lako halijui vizuri anaweza
  kukuomba mchango.
  Aidha michango na sherehe hizi zimekuwa mzigo mkubwa sana kwa baadhi ya
  watu, ikiwa ni pamoja na wale wenye kipato kidogo wanaochangiwa na
  kulazimika kulipa michango hiyo kwa miaka mingi. Je, wajua kuwa kuna
  familia ambazo zimefikia kulazimisha ndugu wauze mashamba au mifugo mtaji
  ili kupata fedha za kuchangia sherehe?. Je, wajua kuwa kuna watu ambao
  zaidi ya nusu ya kipato chao wanatumia kuchangia sherehe na huku
  wakishindwa kulipia huduma muhimu kama shule, matibabu, lishe, nk. Na kuwa
  wakati mwingine wewe au mimi (au wengine kama mimi na wewe) ndio wenyeviti
  na makatibu wa sherehe hiyo?. Na ni sisi tunaoona fahari ya kutumia
  milioni 30 au zaidi kwenye sherehe usiku mmoja?
  Kuna kijana mmoja jamaa yetu juzi juzi alipata shule Australia akawa
  anatafuta mchango wa dola 5,000 aende. Alipata 2,000 na amwekwama kwenda.
  Mwaka kesho akisema anaoa tutamchangia milioni 15-20!!!. Hii si hadithi,
  ni ukweli, na ni kielelezo cha ulimbukeni tuliofikia.
  Siku za karibuni nimetambua kuwa kuna kundi kubwa tu linasikitishwa na huu
  mwenendo, na hata kutambua kuwa tunaweza kuwa tunaandikiwa dhambi kubwa
  (na hukumu yatusubiri) kwa jinsi wengi wetu tunashindwa kusaidia mambo ya
  msingi lakini tunakuwa wepesi kutoa kwenye sherehe.

 • 03:00

  DENZEL HOSTS RADIO VETERAN LEONARD MBOTELA "JE, HUU NI UNGWANA...???"

  in Social Networking

  Je,huu ni ungwana...??? Leonard "Mambo“ Mbotela ni mtangazaji mashuhuri wa redio nchini Kenya. Amejulikana kote nchini kutokana na huduma yake ya zaidi ya miaka 40 tangu 1964. Alikuwa mtangazaji wa habari na michezo hasa soka. Tangu 1966 amekuwa hewani na programu yake "Je, hii ni ungwana?".

  Leonard Mbotela alizaliwa huko Freretown, Mombasa katika familia ya kianglikana ya watoto nane. Babake James Mbotela alikuwa kati ya walimu wa kwanza Waafrika katika Kenya, mamake Ida alifanya kazi ya ustawi wa jamii.

  Leonard alisoma shule ya msingi ya Freretown kati ya 1948 na 1953 halafu Buxton shule ya kati Mombasa 1954 hadi 1958 akaendelea shule ya sekondari ya Kitui High School 1959 hadi 1963.

  Alipata nafasi ya kuingia katika ukurufunzi wa Sauti ya Kenya akishirikiana na Simon Ndesanjo katika programu ‘Hodi hodi mitaani’. 1964 aliajiriwa kama mtangazaji wa huduma ya Kiswahili. Mbotela alianzisha programu yake ya ‘Salamu za vijana’ pia akasoma taarifa za habari za huduma ya Kiswahili.

  Mwaka 1966 alianzisha ‘Je, huu ni ungwana?’ ambayo ni programu ya pekee inayoendelea hadi leo (2006). Alijulikana zaidi nchini kama mtangazaji wa soka kuanzia mwaka 1967. Kati ya programu zake zilizopendwa ni Uhalifu Haulipi, Ongea Lugha Sanifu and Waliosifika.

  Wakati wa uasi wa 1982 (jaribio la kijeshi la kupindua serikali ya rais Moi) Mbotela alilazimishwa kusoma habari za waasi kwa sababu sauti yake ilijulikana kote nchini.

  Katika maisha yake ya kazi alikuwa pia mhusika wa huduma ya "Presidential Press Service" chini ya Rais Moi kwa miaka saba.

  Alirudi KBC akastaafu mwaka 1997 akiwa na cheo cha mwangalizi mkuu wa programu za redio.

  Hata baada ya kustaafu ameendelea kusikika redioni akisoma habari na programu yake "Je hii ni ungwana?".

  Mbotela amemwoa Alice Mwikali mwaka 1970 akazaa naye watoto 3 : Ida, Jimmy na George.

Loading...
Loading...