Our Terms of Use and Privacy Policy have changed. We think you'll like them better this way.

REMEMBERING THE LATE DR.REMMY ONGALA

  • Broadcast in Social Networking
Denzel Musumba

Denzel Musumba

×  

Follow This Show

If you liked this show, you should follow Denzel Musumba.
h:106267
s:1377606
archived
Mwanamuziki mkongwe nchini Tanzania, Dr.Remmy Ongala,amefariki dunia.Kwa wiki kadhaa,Dr.Remmy alikuwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari.Mipango ya mazishi inafanyikia nyumbani kwa marehemu Sinza(Sinza kwa Remmy) jijini Dar-es-salaam.Pumzika kwa amani Dr.Remmy Ongala BC iliwahi kuandika kwa kirefu historia ya Dr.Remmy Ongala.Bonyeza hapa kuisoma historia ya mkongwe huyu wa muziki ambaye mchango wake katika muziki na katika kuitangaza Tanzania kimataifa ni mkubwa na ambao hautokaa usahaulike. Historia ya Marehemu. Alipozaliwa wazazi wake walimuita Ramadhani Mtoro Ongala. Alizaliwa mwaka 1947 katika mkoa wa Kivu huko Democratic Republic of Congo ya leo ambayo hapo zamani kwanza iliitwa Belgian Congo kabla ya kuitwa Zaire. Familia yake iliishi katika eneo lililoitwa Kindu eneo ambalo halikuwa mbali sana kutoka mpakani na Tanzania. Baba yake alikuwa ni mwanamuziki mashuhuri pia akiwa mpiga ngoma kwa kutumia mkono na pia mbira. Pindi tu alipozaliwa familia yake ilihamia Kisangani.

Comments